• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 23, 2018

  UJERUMANI YAFUFUA MATUMAINI YA KUTETEA KOMBE LA DUNIA

  Toni Kroos akikimbia kushangilia baada ya kuwafungia bao la ushindi mabingwa watetezi, Ujerumani dakika ya 90 na ushei wakiichapa Sweden 2-1 katika mchezo wa Kundi F Kombe la Dunia leo Uwanja wa Olimpiki mjini Sochi. Hiyo ni baada ya Ola Toivonen kuanza kuifungia Sweden dakika ya 32 na Marco Reus kuisawazishia Ujerumani ambayo ilimpoteza Jerome Boateng aliyetolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 81 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UJERUMANI YAFUFUA MATUMAINI YA KUTETEA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top