• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 21, 2018

  REFA AOMBA JEZI YA RONALDO AKICHEZESHA MECHI NA MOROCCO

  REFA Mark Geiger aliyechezesha mchezo wa Kundi B Kombe la Dunia jana kati ya Morocco na Ureno amedaiwa kumuomba jezi Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo wakati mchezo ukiendelea.
  Madai hayo yametolewa na kiungo wea Morocco, Nordin Amrabat anayechezea  Watford ya England baada ya mchezo wsa jana timu yake ikichapwa 1-0 kwa bao pekee la Ronaldo
  Nyota wa Real Madrid, Ronaldo jana amefunga bao lake la nne katika mashindano haya baada ya mechi mbili, Ureno ikifikisha pointi nne sawa na Hispania na kuongoza pamoja Kundi B.

  Mark Geiger amedaiwa kumuomba jezi Cristiano Ronaldo wakati wa mchezo dhidi ya Morocco jana 
  "Sifahamu alikuwaje, lakini alikuwa anavutiwa mno Cristiano Ronaldo, na nilimsikia Pepe anasema kwamba alimuomba jezi (Ronaldo) kipindi cha kwanza," alisema Amrabat ambaye alicheza jana licha ya kuumia kwenye mchezo wa kwanza. 
  "Tunazungumzia nini? Kwenye Kombe la Dunia? Si mahala pake hapa.’
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REFA AOMBA JEZI YA RONALDO AKICHEZESHA MECHI NA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top