• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 28, 2018

  YONDAN AANZA KUJIANDAA NA MAISHA BAADA YA SOKA, AFUNGUA DUKA LA VIATU INSTA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI mkongwe wa kimataifa wa Tanzania, Kelvin Patrick Yondan ameanza kujiandaa na maisha baada ya soka kufuatia kuanzisha biashara ya kuuza viatu.
  Yondan ametumia akaunti yake ya Instagram kutangaza biashara yake ya viatu anavyouza huku akiweka na namba ya simu ambayo wateja watakaohitaji watapiga kuvipata.
  Beki huyo wa Yanga SC, pamoja na kuonekana mtukutu uwanjani, lakini nje ya Uwanja amekuwa na maisha yenye kueleweka akiwa ametulia na familia yake.
  Ni mkazi wa Kigamboni akiwa amejenga nyumba huko, eneo la Kibada na rafiki wake wa karibu zaidi ni kiungo wa Simba SC, Mwinyi Kazimoto ambao urafiki wao ulianzia tangu wanacheza chandimu eneo la Kirumba, Mwanza.
  Kelvin Yondan (kulia) akiwa na mchezaji mwenzake wa Yanga, Hassan Kessy na picha ya chini ni tangazo la biashara yake Instagram

  Na wote wamewahi kucheza pamoja Simba SC kabla ya Yondan kuhamia Yanga Juni mwaka 2012 kabla ya Kazimoto kucheza kwa misimu miwili  Al Markhiya in the Qatari kuanzia mwaka 2013.
  Yondan alisajiliwa kama mchezaji chipukizi Simba SC mwaka 2007 akitokea klabu ya Toto African ya Mwanza na Juni 2012 akasajiiwa Yanga kwa dau la Sh. Milioni 30 na mshahara wa Sh 800,00 kwa mwezi ambao sasa umepanda hadi Sh. Milioni 2.
  Pamoja na kuwa beki tegemeo wa Yanga kwa sasa kiasi kwamba Simba SC inataka kumrejesha kuimarisha ukuta wake, lakini pia Yondan ni beki tegemeo wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa sasa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YONDAN AANZA KUJIANDAA NA MAISHA BAADA YA SOKA, AFUNGUA DUKA LA VIATU INSTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top