• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 19, 2018

  SIMBA YAVULIWA UBINGWA WA KOMBE LA UHAI, FAINALI NI MTIBWA NA STAND UNITED

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  SIMBA SC imevuliwa ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Kombe la Uhai inayoshirikisha vikosi vya pili vya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Nusu Fainali viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Lakini haikuwa kazi nyepesi kwa Simba SC kuvuliwa ubingwa, kwani Mtibwa Sugar walilazimika kupigana kwa dakika 120 kufanikisha zoezi hilo na shujaa wao alikuwa ni Abuu Yohana aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 117.
  Na kwa ujumla haikuwa siku nzuri kwa timu za Dar es Salaam, kwani washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam FC nao wametupwa nje pia hii leo.

  Azam FC wamefungwa 1-0 nao na Stand United, bao pekee la Maurice Mahela dakika ya 32 viwanja vya UDOM na sasa fainali itazikutanisha Mtibwa Sugar na timu hiyo ya Shinyanga Juni 21.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA YAVULIWA UBINGWA WA KOMBE LA UHAI, FAINALI NI MTIBWA NA STAND UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top