• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 27, 2018

  MSHAMBULIAJI WA IVORY COAST, WILFRIED BONY WA SWANSEA CITY ATUA DAR KUWEKEZA KATIKA SANAA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZAJI Wilfried Bony wa Klabu ya Swansea City ya England yupo nchini kwa ziara fupi ambapo amesema anatarajia kuwekeza katika sanaa kwa wasanii wa hapa Tanzania.
  Bony ambaye anamalizia ziara yake ya siku nne chini, amesema anavutiwa na kazi za sanaa zinazofanyika nchini, hivyo ameamua kuwekeza kwa ujenzi wa studio ya kisasa na maktaba ya muziki pia kiwanda cha filamu.
  Bony raia wa Ivory Coast yupo nchini kwa ushirikiano na Mtanzania anayeishi nchini England, Jasmine Razack ambaye anahusika na Taasisi ya Uzalendo Kwanza.
  Wilfried Bony akiwa kwenye pantoni ya Kigamboni katika ziara yake ya Tanzania  

  “Navutiwa na kazi za sanaa za Tanzania hasa muziki japokuwa nyingi zimetumia lugha ya Kiswahili, nazipenda nyimbo za Tanzania pia nazijua na huwa nazifuatilia sana.
  “Wengi wanaweza kushangaa kwa kuwekeza kwangu katika sanaa ya filamu na muziki badala ya soka, haya ni mapenzi yangu kwa muziki na filamu baadaye naweza kufikiria kuwekeza katika soka,” alisema Bony.
  Akiwa nchini, Bony amefanya ziara ya utalii katika hifadhi na mbuga mbalimbali za wanyama pia ametembelea vivutio vingine vya utalii nchini ikiwmo visiwa vya Zanzibar.
  Bony mwenye umri wa miaka 29 kabla ya kutua Swansea City amewahi kucheza katika Klabu za Sparta Prague, Vitesse, Manchester City na Stoke City.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI WA IVORY COAST, WILFRIED BONY WA SWANSEA CITY ATUA DAR KUWEKEZA KATIKA SANAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top