• HABARI MPYA

  Thursday, October 12, 2017

  KOCHA MROMANIA WA AZAM ANACHOTAKA NI KUWADUNDA TU MWADUI JUMAMOSI

  Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
  KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amesema kwamba kikosi chake kimewasili mkoani Shinyanga kwa lengo moja tu la kushinda mchezo dhidi ya Mwadui na kuzoa pointi zote tatu Jumamosi hii.
  Kikosi cha Azam FC kimewasili salama mkoani humo jioni ya leo kikitokea mkoani Dodoma kilipopata mapumziko ya muda mfupi, ambapo kwa mujibu wa programu ya kocha huyo wachezaji watafanya mazoezi ya kwanza Shinyanga kesho jioni kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
  Cioaba amesema kwamba kikosi chake kimetua mkoani hapa kikiwa na morali kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.
  Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba amesema anataka ushindi Jumamosi hii dhidi ya Mwadui

  “Wachezaji wote wapo tayari hakuna mchezaji majeruhi na morali ipo juu, wote tunaamini kama tutafanya kazi kama familia huku tukiweka tahadhali kwa wapinzani wetu, huwa nawaambia kuwa timu zote zinacheza mpira mzuri haijalishi ni Yanga ama timu yoyote, cha msingi ni kumuheshimu mpinzani na mchezo wenyewe, ninachohitaji ni ushindi siku ya Jumamosi na kupata pointi tatu,” alisema.
  Mchezaji pekee ambaye ameshindwa kusafiri na kikosi hicho ni kiungo mkabaji Stephan Kingue, ambaye bado hajapona vizuri majeraha ya mgongo huku winga Joseph Kimwaga na mshambuliaji Shaaban Idd, wakiendelea na matibabu baada ya wote kufanyiwa upasuaji hivi karibuni nchini Afrika Kusini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA MROMANIA WA AZAM ANACHOTAKA NI KUWADUNDA TU MWADUI JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top