• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 25, 2017

  SINGIDA UNITED WADHAMIRIA KUREJEA NAMFUA NOVEMBA 4

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Singida United umedhamiria kuanza kuutumia Uwanja wake wa Namfua mkoani Singida kwa mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Novemba 4, mwaka huu.  
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba baada ya ukarabati wa kiwango cha juu, uliohusisha pia eneo la kuchezea mpira (pitch), Namfua sasa upo tayari kwa matumizi.
  Festo amesema kwamba baada ya Uwanja huo kukamilika, Singida United FC wataanza kutumia Namfua Novemba 4 katika mchezo wao dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Yanga.
  Huu ni Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambao Singida United imekuwa ikiutumia katika mechi zake za mwanzo za msimu ambao nao sasa umefungwa kwa ukarabati

  “Ushirikiano wa TFF na Bodi ya Ligi kuhakikisha Namfua unaanza kutumika ni wa kiwango cha juu, viongozi wakuu wa soka nchini wanafanya kazi bega kwa bega na uongozi wa Singida United kuhakikisha kipute cha Ligi Kuu kinaanza kutimka pale Namfua,”amesema Festo.
  Historia ya timu ya Singida United inaanzia kwenye timu nguli kipindi hicho ikijulikana kama Mto Singida FC na inashiriki Ligi Kuu kwa mara ya pili baada ya kupanda msimu huu, kufuatia awali kucheza ligi hiyo miaka ya 2000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED WADHAMIRIA KUREJEA NAMFUA NOVEMBA 4 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top