• HABARI MPYA

  Thursday, October 12, 2017

  WENGER ADANGANYIKA NA HABARI FEKI ZA WEAH KUSHINDA URAIS LIBERIA

  Nyota wa zamani wa AC Milan, George Weah anasubiri matokeo ya uchaguzi wa Urais Liberia kuwania kumrithi Ellen Johnson Sirleaf 

  KLABU ALIZOCHEZEA GEORGE WEAH 

  1985–1986 Mighty Barrolle
  1986–1987 Invincible Eleven
  1987 Africa Sports
  1987–1988 Tonnerre Yaounde
  1988–1992 Monaco 103
  1992–1995 Paris Saint-Germain
  1995–2000 Milan
  2000 → Chelsea (loan) 
  2000 Manchester City
  2000–2001 Marseille 
  2001–2003 Al-Jazira  
  KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amedanganyika na habari feki zinazoenezwa kwamba George Weah ameshinda Urais wa Liberia.
  Wenger, ambaye alimgundisha mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 51 katika klabu ya Monaco kuanzia mwaka 1988 hadi 1992, ametumia tovuti ta The Gunners kumpongeza Weah. Kwa bahati mbaya, Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 67, matokeo halisi hayajatangazwa.
  Wenger amesema, “Ningependa kumpongeza mmoja wa wachezaji wangu wa zamani, ambaye amekuwa Rais wa Liberia, George Weah.
  Weah, Mwanasoka Bora wa zamani wa Mwaka wa FIFA, anawania tena Urais wa Liberia katika uchaguzi uliofanyika Jumanne baada ya kushindwa katika chaguzi mbili za awali.
  Arsene Wenger (kulia) akiwa na George Weah wakati wanafanya naye jazi Monaco kati ya mwaka 1988 na 1992

  Weah anabaki kuwa Mwanasoka pekee Mwafrika aliyeshinda tuzo yaBallon d'Or mwaka 1995.
  Ni Wenger alimvuta Weah Ulaya mwaka 1988 alipomnunua Monaco akitokea Tonnerre Yaounde ya Cameroon. Kabla ya hapo alicheza Mighty Barrolle, Invincible Eleven za kwao Liberia na Africa Sports ya Ivory Coast.
  Alijiunga na Paris Saint-German ya Ufaransa mwaka 1992, ambako alicheza kwa misimu mitatu kabla ya kuhamia AC Milan ya Italia.
  Amecheza pia Chelsea kwa mkopo, Manchester City zote za England, Marseille ya Ufaransa na Al-Jazira ya Saudi Arabia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENGER ADANGANYIKA NA HABARI FEKI ZA WEAH KUSHINDA URAIS LIBERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top