• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 29, 2017

  SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA JANA UWANJA WA UHURU

  Kiungo wa Yanga, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi akipasua katikati ya wachezaji wa Simba, Muzamil Yassin (kulia) na Emmanuel Okwi (kushoto) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam timu hizo zikitoka sare ya 1-1 
  Mfungaji wa bao la Yanga jana, Obrey Chirwa (kushoto) akiwatoka wachezaji wa Simba, 
  Mfungaji wa bao la Simba jana, Shiza Kichuya (kushoto) akimtoka beki wa Yanga, Gardiel Michael
  Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib (kulia) akimtoka kiungo wa Simba, Muzamil Yassin
  Beki wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' (kulia) akiwa ameondosha mpira kwenye himaya ya kiungo wa Yanga, Pius Buswita 
  Beki wa Simba, Erasto Nyoni akiruka kwa staili ya kung-fu dhidi ya winga wa Yanga, Geoffrey Mwashiuya
  Beki wa Yanga, Kevin Yondan, Emmanuel Okwi akimdhibiti mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi  
  Beki wa Yanga, Juma Abdul (kushoto) akiokoa dhidi ya kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima
  Kikosi cha Yanga katika mchezo jana 
  Kikosi cha Simba katika mchezo wa jana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA JANA UWANJA WA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top