• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 25, 2017

  TENGA MAKAMU, KARIA, LINA NA MAREALLE WAJUMBE KAMATI ZA CAF

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chilla Tenga ameteuliwa kwenye Kamati mbili tofauti za Shirikisho la Soka Afrika CAF.
  Taarifa ya CAF kwa Bin Zubeiry Sports – Online imesema kwamba, Tenga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CAF, sasa amaingia kwenye Kamati za Maendeleo ya Futsal na Soka la Ufukweni na Kamati ya Ufundi na Maendeleo.
  Mbali na Tenga, Watanzania wengine watatu wameingizwa kwenye Kamati za CAF akiwemo Rais wa sasa wa TFF, Wallace Karia aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
  Rais wa zamani wa TFF, Leodegar Tenga ameteuliwa kwenye Kamati mbili tofauti za CAF

  Wengine ni Kaimu Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Lina Mhando aliyeteuliwa kwenye Kamati ya Maandalizi ya Soka la Wanawake na Dk. Paul Gaspar Marealle aliyeteuliwa Kamati ya Tiba.
  Katika Kamati Kuu, Rais ni Ahmad wa Madagascar, Makamu wa kwanza ni Kwesi Nyantakyi wa Ghana, Makamu wa pili Constant Omari Selemani wa DRC na Makamu wa tatu ni Fouzi Lekjaa wa Morocco, wakati mbali na Tenga Wajumbe wengine ni Adoum Djibrine (Chad), Hani Abo Rida (Misri), Almamy Kabele Camara (Guinea), Tarek Bouchamaoui (Tunisia), Kalusha Bwalya (Zambia), Lydia Nsekera (Burundi), Alexander Danny Jordaan (Afrika Kusini), Amaju Melvin Pinnick (Nigeria), Hassan Musa Bility (Liberia), Isha Johansen (Sierra Leone), Rui Eduardo da Costa (Angola), Suleiman Hassan Waberi (Djibouti), Ahmed Yahya (Mauritania), Moses Magogo (Uganda) na Essam Ahmed wa Misri, ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu. 
  Katika Kamati ya Futsal na Soka la Ufukweni, Tenga ni Makamu wa Rais chini ya Rais, Moses Magogo wa Uganda na Wajumbe Virginia Mendes Da Cruz wa Guinea Bissau, Khiba Mohoanyane wa Lesotho, Hussein Abdunnaser Ahmed wa Libya, Abilio Espirito Santo wa Sao Tome, Oumarou Fadil wa Cameroon, Abdoulaye Saydou wa Senegal, Ali Harred Mohamed wa Djibouti, Felix Ansong wa Ghana, Khaled Latif wa Misri, Lombe Mbalashi wa Zambia, Mahaforona Cyril wa Madagascar, Omega Sibanda wa Zimbabwe, Pascal da Fonseca Loforte wa Msumbiji, Pasipononga Liwewe wa Zambia, Poobalan Govindasamy wa Afrika Kusini na Senator Obinna Ogba wa Nigeria.
  Kamati ya Ufundi na Maendelezo Tenga ni Makamu wa Rais pia, chini ya Rais, mcheΩaji mwenzake wa zamani barani, Kalusha Bwalya wa Zambia na Wajumbe, Adoum Djibrine wa Chad, Suleiman Hassan Waberi wa Djibouti, Malouche Belhassan wa Tunisia, Fran Smith wa Afrika Kusini, Nasser Larguet wa Morocco, Watson Suubi Edgar wa Uganda, Khalilou Fadiga wa Senegal, Alshelmani Abdulhakim wa Libya, Korichi Taoufique wa Algeria, Jeremie Njitap wa Cameroun, Ilonga Erita wa DRC, Ahmed Yussuf Fresh wa Nigeria, Ahmedou Mbourick wa Mauritanie), Hazem Imam wa Misri na Jean Michel Bennezet.
  Katika Kamati ya CHAN, Karia ni Mjumbe chini ya Rais Hassan Musa Bility wa Liberia na Makamu wa kwanza, Rui Eduardo da Costa wa Angola na Makamu wa pili, Wadie Jary na Lina kwenye Kamati ya Soka la Wanawake yupo chini ya Rais, Isha Johansen wa Sierra Leone na Makamu wake, Lydia Nsekera wa Burundi wakati Dk Marealle kwenye Kamati ya Tiba yupo chini ya Rais Adoum Djibrine wa Chad na makamu wake, Yacine Zerguini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TENGA MAKAMU, KARIA, LINA NA MAREALLE WAJUMBE KAMATI ZA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top