• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 27, 2017

  BARUAN MUHUZA AULA TENA KAMATI YA UENDESHWAJI LIGI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI mpya wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Clement Sanga amemrejesha Meneja wa Michezo wa Azam TV, Baruan Muhuza kwenye Kamati mpya ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi. 
  Kamati hiyo itaongozwa na yeye mwenyewe, Sanfa akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti, Shani Mligo, Katibu Boniface Wambura na Wajumbe Issa Batenga, Leslie Liunda, Wakili Saleh Njaa, Dk Ellyson Maeja, George Malawa, Isaac Chanji, Mbakileki Mutahaba na Ally Mayay. 
  Kamati hiyo ya TPLB ndiyo inayoshughulikia uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Ligi Daraja la Pili (SDL). 
  Meneja wa Michezo wa Azam TV, Baruan Muhuza amerejeshwa kwenye Kamati Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi

  Pia Mwenyekiti ameteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB. Wajumbe hao ni Kanali Charles Mbuge ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Ruvu Shooting, na Abuu Changawa 'Majeki'. 
  Kwa mujibu wa Ibara ya 28(vi) ya Kanuni za Uendeshaji (Governing Regulations) za TPLB, Mwenyekiti ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi.
  Akizungumzia uteuzi wake, Muhuza amesema; "Kwanza namshukuru sana Mwenyekiti kwa kuniamini na kuamua kuniacha niendelee kuwa mjumbe wa Kamati hii nyeti, ambayo ina jukumu zito na la muhimu,". 
  "Nitajitahidi kwa weledi na uwezo aliyonijaalia Mwenyezi Mungu kuhakikisha tunafanya kazi zinazo kusudiwa ili kuusaidia mpira wa nchi yetu,"amesema mtangazaji huyo wa Azam TV.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARUAN MUHUZA AULA TENA KAMATI YA UENDESHWAJI LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top