• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 30, 2017

  MSUVA AENDELEA KUPIKA MABAO DIFAA JADIDA YAUA 3-0 LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, JADIDA
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania jana ameendelea kuwa mpishi mzuri wa mabao kwa timu yake, Difaa Hassan El Jadida ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya  Moghreb Tetouan katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida.
  Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga, Msuva, aliseti mabao ya mawili ya kwanza El Jadida, moja kila kipindi kabla ya kupumzishwa, akimpisha Hamid Ahadad dakika ya 77.
  Mabao ya Difaa jana yamefungwa na Bilal El Magri mawili dakika za 45 na 79, baada ya  Adnane El Ouardy kufunga la kwanza dakika ya saba.
  Simon Msuva akitoa pasi kwenye mchezo wa jana 

  Baada ya mchezo huo, Difaa ina viporo viwili dhidi ya vigogo, FUS Rabat na Wydad Casablanca, ambayo havijapangiwa tarehe. 
  Kikosi cha Difaa Hassan El Jadida jana kilikuwa; Yahia El Filali, Y. Aguerdoum, M. Hadhoudi, Anouar Jayo, Fabrice Ngah, M. Bameammer, Chouaib El Maftoul/Ayoub Nanah dk70, Mario Bernad, Simon Msuva/Hamid Ahadad dk77, Bilal El Magri na Adnane El Quadry/Youness Hawassi dk70. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSUVA AENDELEA KUPIKA MABAO DIFAA JADIDA YAUA 3-0 LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top