• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 28, 2017

  YANGA YAPANGA KIKOSI HAKINA MCHEZAJI HATA MMOJA AMEWAHI KUIFUNGA SIMBA HATA ALIPOKUWA TIMU NYINGINE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Yanga hakina hata mchezaji mmoja amewahi kuifungia Simba hata wakati akiwa na timu nyingine kabla ya kutua Jangwani.
  Yanga inamenyana na Simba Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kocha Mzambia, George Lwandamina hatakuwa na wazoefu wote wa mechi dhidi ya Simba.
  Washambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe wenye uzoefu wa kuifunga Simba wote ni majeruhi na leo Lwandamina amewaanzisha pamoja Ibrahim Ajib na Mzambia Obrey Chirwa.
  Lwandamina ameweka viungo watatu katikati, Mkongo Papy Kabamba Tshitshimbi na wazawa Pius Buswita na Raphael Daudi na winga mmoja, Geofrey Mwashiuya.
  Ibrahim Ajib ataongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga leo dhidi ya Simba

  Safu ya ulinzi inaundwa na kipa Mcameroon Youthe Rostand mabeki wazawa Juma Abdul kulia, Gardiel Michael kushoto na Andrew Vincent ‘Dante’ na Kelvin Yondani katikati.
  Yanga haijaifunga Simba tangu Februari 20, mwaka 2016 iliposhinda 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu, mabao ya Donald Ngoma dakika ya 39 na Amissi Tambwe dakika ya 72.
  Baada ya hapo, mechi nne zilizofuata Yanga walifungwa tatu na kutoka sare mara moja.
  Oktoba 1, mwaka walitoa sare ya 1-1, Amissi Tambwe akianza kuifungia Yanga dakika ya 26, kabla ya Shiza Kichuya kuisawazishia Simba dakika ya 87, kabla ya Januari 10, mwaka huu Wekundu wa Msimbazi kushinda tena kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  
  Februari 26, Simba wakatoka nyuma kwa bao la penalti la Simon Msuva dakika ya tano na kushinda tena Simba 2-1 kwa mabao ya Mrundi Laudit Mavugo dakika ya 66 na Kichuya dakika ya 81, kabla ya Agosti 23, mwaka huu kushinda tena kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.
  Yanga SC; Youthe Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Papy Kabamba Tshitshimbi, Pius Buswita, Raphael Daudi, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib na Geofrey Mwashiuya.
  Benchi; Beno Kakolanya, Hassan Kessy, Mwinyi Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Pato Ngonyani, Yussuf Mhilu na Emmanuel Martin.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA YAPANGA KIKOSI HAKINA MCHEZAJI HATA MMOJA AMEWAHI KUIFUNGA SIMBA HATA ALIPOKUWA TIMU NYINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top