• HABARI MPYA

    Tuesday, October 24, 2017

    MAYANGA AWAREJESHA MAGURI NA FARID MUSSA TAIFA STARS KUIVAA BENIN NOVEMBA 11

    Na Aisha Mohammed, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga amewarejesha kikosini kiungo Farid Mussa na mshambuliaji, Elias Maguri kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa mapema mwezi ujao.
    Baada ya kucheza nyumbani mfululizo mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars sasa itatoka mwezi ujao kwenda Benin kucheza na wenyeji Novemba 11, mwaka huu.
    Na Mayanga leo ameita kikosi cha wachezaji 24 ambacho kitaingia kambini Novemba 5 mjini Dar es Salaam kabla ya kusafiri Novemba 9 kwenda Benin tayari kwa mchezo huo.  
    Elias Maguri (kushoto) akiwa na Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro' 

    Na ndani yake amewaorodhesha Maguri aliyekuwa anacheza Oman na Farid Mussa anayecheza Tenerife B ya Hispania, ambao wote hakuwaita kwenye mchezo uliopita dhidi ya Malawi, uliomalizika kwa sare ya 1-1 Oktoba 7, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
    Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United) na Ramadhani Kabwili, mabeki Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afruka Kusini), Gardiel Michael (Yanga), Kevin Yondan (Yanga), Nurdin Chona (Prisons), Erasto Nyoni (Simba) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).
    Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba), Raphael Daudi (Yanga), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Ibrahim Hajib (Yanga), Mohammed Issa (Mtibwa), Farid Mussa (Tenerife/Hispania) na Abdul Mohammed (Tusker/Kenya) na washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Azam FC), Elias Maguri (Huru) na Yohanna Nkomola (Huru).   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAYANGA AWAREJESHA MAGURI NA FARID MUSSA TAIFA STARS KUIVAA BENIN NOVEMBA 11 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top