• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 27, 2017

  VIGOGO ARSENAL, MAN UNITED NA LIVERPOOL WAKUTANA MAREKANI

  VIONGOZI wakuu wa klabu za asili ya England, Arsenal, Manchester United na Liverpool — wamekutana kwa mazungumzo mjini New York, Marekani kuimarisha umoja wao.
  Walipata chakula cha usiku kwa pamoja katika mgahawa wa Kitaliano, Locanda Verde uliopo wilaya ya Tribeca wiki iliyopita, Arsenal ikiwakilishwa na Mtendaji wake Mkuu, Ivan Gazidis, Liverpool ikiwakilishwa na mmiliki wake, John W Henry, Manchester United alikuwepo Makamun Mwenyekiti, Ed Woodward na ndugu wawili watoto wa mmiliki, Glazer Avram na Joel.
  Hawakutaka kufanya siri juu ya kikao chao, walitafuta sehemu maarufu na ya wazi na kuketi kwa mazungumzo yao, huku wakiendelea na chakula cha jioni hadi wakapigwa picha na shabiki wa Arsenal.

  Wakuu wa Manchester United, Arsenal na Liverpool walikutana kwa chakula cha usiku mjini New York hivi karibuni PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Ilionekana kama mazungumzo yao yalihusu mgawanyo wa malipo ya haki za Televisheni katika Ligi Kuu ya England, zikiwa zimebaki siku saba kabla ya kikao cha pili cha klabu zote. 
  Kikao  hicho kiliahirishwa baadaye kwa sababu klabu 20 hazikuafikiana — 11-9 zikipinga mabadiliko yanayotakiwa na timu kubwa sita, wakati 14-6 wanahitaji.
  Lakini umoja wa timu tatu kubwa 'Big Three' kwenye Big Apple unabadilisha muundo, kwani tayari inajulikana kuna Big Six wanaopigania mgawo mkubwa wa fedha za matangazo ya Televisheni.
  Arsenal wanasema Gazidis alikuwa New York kuonana na mmiliki Stan Kroenke na kukawa na kikao cha chakula cha jioni kujadili mambo ya NFL. 
  United wanasema Woodward alikutana na watoto wa Glazers kujadilia masuala hayo hayo ya NFL, wakati Henry alikuwa hapo kwa masuala ya Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VIGOGO ARSENAL, MAN UNITED NA LIVERPOOL WAKUTANA MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top