• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 29, 2017

  JOSHUA AMSHINDA KWA TKO TAKAM RAUNDI YA 10

  Anthony Joshua akimuangalia mpinzani wake, Carlos Takam anavyopepesuka kwa kipigo alichompa katika pambano la uzito wa juu usiku huu Uwanja wa Principality mjini Cardiff, Uingereza. Joshua ameshinda kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya 10 na kutetea taji lake la IBF baada ya refa kusimamisha pambano kumuokoa Takam aliyekuwa anatokwa damu nyingi usoni kufuatia kuchanika juu ya jicho mwanzoni mwa pambano. Ikumbukwe Takam alipewa nafasi ya kupigana katika pambano hili siku 12 kabla, kufuatia Kubrat Pulev kujitoa baada ya kuumia mazoezini na Joshua alikutwa ana uzito mkubwa zaidi ya mpinzani wake walipopimwa juzi 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JOSHUA AMSHINDA KWA TKO TAKAM RAUNDI YA 10 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top