• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 30, 2017

  MEJA MINGANGE ACHUKUA NAFASI YA IDDI CHECHE AZAM U-20

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa zamani wa Ndanda FC na Mbeya City, Meja Mstaafu, Abdul Mingange leo ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Azam FC.
  Mingange anachukua nafasi ya Idd Nassor Cheche, ambaye tangu Januari mwaka huu amepandishwa kuwa kocha Msaidizi wa timu ya wakubwa, chini ya Mromania, Aristica Cioaba.  
  Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema kwamba Mingange ni kocha mzofu na mwenye rekodi nzuri ya kufanya kazi na wachezaji vijana.
  Meja Mstaafu, Abdul Mingange ndiye kocha mpya U-20 ya Azam FC


  “Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC kwa pamoja na uongozi, imezingatia sifa za Meja Mingange kulingana na mahitaji ya klabu kwa mwalimu wa U-20. Niseme tu kwamba, tuna matarajio makubwa kwa Meja Mingange,”amesema Maganga.
  Pamoja na hayo, Maganga amesema uongozi umeridhishwa na maendeleo ya Iddi Cheche kama kocha Msaidizi wa timu ya wakubwa.
  “Pia uongozi umefurahishwa na utendaji mzuri wa Cheche kama kocha Msaidizi na unamtakia kila la heri,”amesema.
  Kwa upande wake, akizungumzia kupewa nafasi hiyo, Mingange alisema kuwa kwa muda wa mwezi mmoja hadi miwili ijayo, timu hiyo itakuwa na mtazamo tofauti chini yake tofauti na ilivyo sasa huku akiweka wazi kushirikiana na watangulizi wake waliokuwa wakikinoa kikosi hicho.
  “Kwanza ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata bahati ya kuja kuwepo kwenye timu ya Azam FC hasa kwenye timu ya vijana kwa sababu mimi napenda sana kufundisha vijana na nilishafanya hivyo miaka iliyopita, kwa hiyo kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hiyo kwa kujumuika katika klabu kubwa kama hii yenye kila kitu katika mpira wa Tanzania.
  “Lakini vile vile nafikiri uongozi wameona juhudi zangu katika sehemu hizo nilizopita na wameona sifa nilizonazo naweza kidogo nikaongeza jambo hapa kwenye timu yetu kwa hilo tu nasema na mimi nitajitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuhakikisha timu yetu ya vijana infanya vizuri na tunaweza kupandisha vijana wakeongeza nguvu kwenye timu yetu kubwa,” alisema Mingange. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MEJA MINGANGE ACHUKUA NAFASI YA IDDI CHECHE AZAM U-20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top