• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 31, 2017

  NDUNDA ‘AJIACHIA’ NA NIMAA MCHUMBA WA ZAMANI WA MANYIKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIPA mpya wa Simba, Said Mohammed ‘Ndunda’ ameposti picha akiwa na mchumba wa kipa wa zamani wa klabu hiyo Peter Manyika, aitwaye Naima Salum ‘Nimaa’.
  Ndunda yuko katika msimu wake wa kwanza Simba SC baada ya kujiunga nayo kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  Lakini mlinda mlango huyo bora wa Kombe la COSAFA, amekuwa na mwanzo mbaya Msimbazi baada ya kuumia goti mazoezini katika kambi ya Zanzibar Agosti, mwaka huu, mwezi mmoja tangu asajiliwe.
  Simba ikalazimika kumpeleka India kwa matibabu, ambayo yatamuweka nje ya Uwanja hadi mwakani na wakati huu akiwa anaugulia maumivu ya goti, Nduda ameposti picha kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na ‘shemeji’ yake wa zamani.  
  Nduda (katikati) ameposti picha hii akiwa nan Nimaa (kulia) 
  Katika picha hiyo, Nimaa anaonekana mwenye furaha kwenye eneo la kifua cha kipa wa zamani wa Maji Maji na Yanga.
  Nimaa aliachana na Manyika mwaka jana, kabla ya kipa huyo kuhamia Singida United iliyopanda Ligi Kuu msimu huu ambako aamekwenda kuwa kipa wa kwanza.
  Simba ilivutiwa na Nduda na kumsajili baada ya kudaka vizuri katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa Kombe la COSAFA dhidi ya Lesotho Julai 7, mwaka huu mjini Rusternburg, Afrika Kusini Taifa Stars ikishinda kwa penalti baada ya sare ya 0-0. 
  Na Nduda akashinda tuzo ya kipa bora wa mashindano hayo baada ya kazi yake nzuri kwenye mchezo huo mmoja tu, kiasi cha kuwashawishi na Simba kumsajili na kumuunganisha na kipa namba wa Taifa Stars, Aishi Manula aliyesajiliwa msimu huu pia Msimbazi, kutoka Azam FC.
  Nimaa enzi za penzi lake 'shatashata' na Peter Manyika  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDUNDA ‘AJIACHIA’ NA NIMAA MCHUMBA WA ZAMANI WA MANYIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top