• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 27, 2017

  MBARAKA MCHEZAJI BORA WA SEPTEMBA AZAM, KUKABIDHIWA TUZO LEO KABLA YA MECHI CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Mbaraka Yussuf, ndiye Mchezaji Bora wa Azam FC mwezi Septemba, mwaka huu.
  Yussuf ametwaa tuzo hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi na mashabiki wengi wa soka na kuwazidi wapinzani wake waliokuwa wakishindanishwa naye, kipa Razak Abalora na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
  Jumla ya kura 358 zilipigwa kwenye akaunti rasmi za Azam FC za mitandao ya kijamii ya facebook na instagram, zilizowagusa wachezaji hao watatu waliokuwa waikipiga kura.
  Mbaraka Yussuf (kushoto) ndiye Mchezaji Bora wa Azam FC mwezi Septemba, mwaka huu

  Mshambuliaji huyo akapata takribani asilimia 65 ya kura hizo zote baada ya kuibuka kidedea kwa jumla ya kura 190, akipigiwa 140 kwenye facebook na zile za Instagram zikiwa 50.
  Abalora ameshika nafasi ya pili akizoa jumla ya kura 86, akipata kura 59 facebook na 27 instagram huku Sure Boy akipigiwa jumla ya kura 82 (facebook 65, instagram 17).
  Baada ya kutwaa tuzo hiyo, Yusuph aliyefunga mabao mawili mpaka sasa kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) atakabidhiwa tuzo yake kabla ya kuanza mchezo wa Azam FC dhidi ya Mbeya City leo Uwanja wa Azam Complex Saa 1.00 usiku.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar, anakuwa mchezaji wa pili wa Azam FC kutwaa tuzo hiyo baada ya beki Yakubu Mohammed, kuitwaa kwa mara ya kwanza mwezi Agosti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBARAKA MCHEZAJI BORA WA SEPTEMBA AZAM, KUKABIDHIWA TUZO LEO KABLA YA MECHI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top