• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 30, 2017

  PRISONS YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 NA KUSOGEA ANGA ZA UBINGWA LIGI KUU

  Na Princess Asia, MBEYA
  TIMU ya Tanzania Prisons imejisogeza anga za ubingwa baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo, Mohamed Rashid dakika ya 19, ambaye sasa anafikisha mabao matano sawa na mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib wakimfuatia nyota wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi mwenye mabao nane.
  Faida zaidi ni kwa Prisons inayofikisha pointi 13 sasa sawa na Singida United na kupanda hadi nafasi ya tano, nyuma ya mabingwa wa zamani watupu, Simba, Yanga, Azam na Mtibwa Sugar wenye pointi 16 kila mmoja. 
  Ligi Kuu itaendelea Ijumaa, Maji Maji FC wakiikaribisha Stand United Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wakati Jumamosi Singida watakuwa wenyeji wa Yanga Uwanja wa Namfua, Singida na Ndanda FC wataikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  Mechi nyingine za Jumamosi, Kagera Sugar wataikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Njombe Mji FC wataikaribisha Mbao FC Uwanja wa Saba Saba na Azam FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Jumapili kutakuwa na mechi mbili, mbali na Mbeya City kuwa wenyeji wa Simba, Lipuli FC nao wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PRISONS YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 NA KUSOGEA ANGA ZA UBINGWA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top