• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 29, 2017

  AZAM FC WASEMA MECHI NA MBEYA CITY ILIKUWA SHUGHULI NZITO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LICHA ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City usiku wa juzi, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche, amedai kuwa haikuwa mechi nyepesi kutokana na upinzani mkubwa ulioonyeshwa na wapinzani wao.
  Bao pekee lililoipa Azam FC pointi tatu, lilifungwa na Mchezaji Bora wa Azam FC (NMB Player of the Month) mwezi Septemba-Oktoba, mshambuliaji Mbaraka Yusuph, akitumia vema kona iliyochongwa na winga Enock Atta na mpira kumgonga mgongoni baada ya kumponyoka kipa wa Mbeya City, Owen Chaima.
  Mbaraka Yusuph juzi aliifungia bao pekee Azam FC ikishinda 1-0 dhidi ya Mbeya City 

  Cheche amesema kuwa mechi hiyo ilikuwa na ushindani mkubwa kuanzia mwanzo hadi mwisho huku akidokeza kwamba kama mechi zote za ligi zingekuwa zikichezwa kwa kiwango hicho basi soka la Tanzania lingepiga hatua.
  “Nafurahi kwa ushindi na vile vile nafurahi kwa kiwango na ushindani tuliokutana nao katika mechi, kama tunakuwa tunacheza ligi katika mechi zote kwa namna hii nafikiri kiwango chetu cha mpira Tanzania kingekwenda juu, lakini inatokezea baadhi ya mechi moja moja mechi nyingi zinakuwa na matatizo,” alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC WASEMA MECHI NA MBEYA CITY ILIKUWA SHUGHULI NZITO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top