• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 29, 2017

  SAMATTA AFIKISHA MECHI 69 GENK IKITOA SARE 0-0 UGENINI

  Na Mwandishi Wetu, KORTRIJK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza mechi yake ya 69, timu yake, KRC Genk ikilazimisha sare ya 0-0 na wenyeji, KV Kortrijk katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A, Ubelgiji uliofanyika Uwanja wa Guldensporen mjini Kortrijk.
  Samatta alicheza kwa dakika 70 kabla ya kumpisha Nikolaos Karelis aliyekuwa anarejea uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi.
  Katika mechi hizo 69, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mechi za mashindano yote tangu alipowasili Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Mbwana Samatta (kulia) akipambana katika mchezo wa jana
  Katika mechi hizo, Samatta ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika mwaka jana alipokuwa na Mazembe, 41 ameanza na mechi 24 ametokea benchi.
  Kikosi cha KV Kortrijk kilikuwa: Kaminski, Verboom, Kovacevic, Rougeaux, Attal, D'Haene/Kagé dk84, Vanderbruggen, Azouni, Ajagun, Chevalier and Perbet/Budkivskyi dk72.
  KRC Genk : Vukovic, Uronen, Colley, Aidoo, Mata/Maehle dk74, Heynen, Writers, Malinovskyi/Buffalo dk87, Pozuelo, Samatta/Karelis dk70 na Ingvartsen.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AFIKISHA MECHI 69 GENK IKITOA SARE 0-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top