• HABARI MPYA

  Friday, October 13, 2017

  TYSON FURY ATANGAZA NIA YA KUREJEA ULINGONI MWAKANI

  BONDIA Tyson Fury ameelezea nia yake ya kurejea ulingoni mwakani — ikiwa ni wiki moja tu baada ya kusema hataomba leseni mpya Bodi ya Umiliki wa Masumbwi Uingereza.
  Fury hajapigana tangu amalize utawala wa Wladimir Klitschko wa muda mrefu kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani mjini Dusseldorf mwezi Novemba mwaka 2015. 
  Kufuatia kuwa nje kwa sababu za maumivu kwanza na baadaye kufungiwa kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu, bondia huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa sasa hana leseni baada ya kupokonywa kwa kesi ya utumiaji dawa zilizopigwa marufuku michezoni.


  Tyson Fury amesema anataka kurejea ulingoni kwa kupigana mapambano matatu mwakani PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Lakini wiki moja tu tangu aseme hataomba kurudishiwa leseni na BBBoC, Fury ametweet: "Kuwa tayari kupambana April mwaka 2018 katika pambano kubwa! & tena kwenye majira joto katika pambano kubwa! & tena kurudi mwishoni mwa mwaka. Mapambano matatu makubwa 2018,". 
  Hii si mara ya kwanza Fury anatangaza kurejea ulingoni. Mfalme huyo wa zamani wa uzito wa juu duniani, ambaye alilazimika kuachia mikanda yake kufuatia matatizo yake nje ya ulingo, alirudi gym mapema mwaka huu kwa lengo kubwa la kupigana na Muingereza mwenzake, Anthony Joshua.
  Lakini mipango hiyo ilizimwa na tuhuma zake za kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni na hadi sasa hana leseni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TYSON FURY ATANGAZA NIA YA KUREJEA ULINGONI MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top