• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 28, 2017

  SIMBA YAWAPANGIA YANGA ‘FOWADI YA MAANGAMIZI’...MAVUGO, OKWI, NIYO NA KICHUYA WAANZISHWA PAMOJA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mcameroon wa Simba, Joseph Marius Omog amepanga safu ya ushambuliaji inayoundwa na wachezaji wenye uzoefu wa kuifunga Yanga.
  Simba na Yanga zinamenyana kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Omog amewapanga pamoja washambuliaji Mrundi Laudit Mavugo na Mganda Emmanuel, Okwi.
  Pembeni, Omog anayesaidiwa na kocha Mrundi, Masudi Juma amewapanga viungo washambuliaji Mnyarwanda Haruna Niyonzima na mzawa, Shiza Kichuya.
  Katika safu ya kiungo, Omog amewapanga  James Kotei nq Muzamil Yassin, wakati safu ya ulinzi inaundwa na kipa Aishi Manula, beki wa kulia Erasto Nyoni, kushoto Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na katikati wanacheza Mganda, Juuko Murshid na Mzimbabwe, Method Mwanjali ambaye pia ni Nahodha.  
  Mavugo, Okwi na Kichuya wote wana uzoefu wa kuifunga Yanga – maana yake Omog amepanga safu ya ushambuliaji kikobo ya mahasimu.
  Simba haijafungwa na Yanga tangu Februari 20, mwaka 2016 ilipochapwa 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu, mabao ya Donald Ngoma dakika ya 39 na Amissi Tambwe dakika ya 72.
  Baada ya hapo, mechi nne zilizofuata Wekundu wa Msimbazi walishinda tatu na kutoka sare mara moja.
  Oktoba 1, mwaka walitoa sare ya 1-1, Amissi Tambwe akianza kuifungia Yanga dakika ya 26, kabla ya Shiza Kichuya kuisawazishia Simba dakika ya 87, kabla ya Januari 10, mwaka huu Wekundu wa Msimbazi kushinda tena kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  
  Februari 26, Simba wakatoka nyuma kwa bao la penalti la Simon Msuva dakika ya tano na kushinda tena Simba 2-1 kwa mabao ya Mrundi Laudit Mavugo dakika ya 66 na Kichuya dakika ya 81, kabla ya Agosti 23, mwaka huu kushinda tena kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.
  Kikosi cha Simba SC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Emmanuel Okwi, Laudit Mavugo na Haruna Niyonzima.
  Katike benchi wapo; Emmanuel Mseja, Ally Shomari, Said Ndemla, John Bocco, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto na Nicholas Gyan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA YAWAPANGIA YANGA ‘FOWADI YA MAANGAMIZI’...MAVUGO, OKWI, NIYO NA KICHUYA WAANZISHWA PAMOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top