• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 27, 2017

  HUYU TSHISHIMBI ATAFANYA MAMBO KAMA HAYA TENA NA KESHO?

  Kiungo Mkongo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi akimuacha winga wa Simba, Shiza Kichuya katika mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba ilishinda kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 
  Tshishimbi aling'ara mno akiichezea Yanga kwa mara ya kwanza baada ya kusajiliwa kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland
  Na aliingia kwenye mchezo huu baada ya kufanya mazoezi na wenzake kwa siku mbili tu kisiwani Pemba 
  Tshishimbi hapa aamgeuza 'mtu mzima' Emmanuel Okwi kwenye boksi

  Hapa ni yeye na wao; Tshishimbi dhidi ya wachezaji wengi wa Simba 
  Tshishimbi pia alikaribia kufunga kama si kipa wa Simba, Aishi Manula kuuwahi mpira hapa. Je, kesho atang'ara tena timu hizo zikikutana katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru? 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HUYU TSHISHIMBI ATAFANYA MAMBO KAMA HAYA TENA NA KESHO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top