• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 24, 2017

  SIMBA WAFURAHIA KAMBI NZURI MTONI MARINE, HOTELI YA KISASA ZAIDI ZANZIBAR

  Na Salim Vuai, ZANZIBAR
  SIMBA SC inafurahia kambi nzuri katika hoteli ya Mtoni Marine visiwani Zanzibar wakijiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Nyasi bandia za Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam zinatarajiwa kutimbika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya wapinzani wa kihistoria, Simba na Yanga Jumamosi. 
  Na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Sunday Manara amesema leo visiwani Zanzibar kwamba kikosi chao kipo katika kambi nzuri Mtoni Marine, hoteli yenye hadhi nyota saba.
  Hii ndiyo hoteli ya Mtoni Marine ambako Simba imeweka kambi visiwani Zanzibar  
  Amesema pamoja na kambi, vijana wanaendelea vyema na mazoezi asubuhi na jioni chini ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog anayesaidiwa na Mrundi, Masudi Juma na mzawa, Muharammi Mohammed ‘Shilton’, kocha wa makipa.   
  Hata hivyo, Manara zaidi ya kufurahia kambi na maandalizi, hakutaka kama kawaida yake kutoa majigambo kuelekea mchezo wa Jumamosi, akisema tu dakika 90 zitatoa majibu.
  Simba ipo Zanzibar tangu mapema jana baada ya mchezo wao wa Jumamosi wa Ligi Kuu pia dhidi ya Njombe, wakishinda 4-0 Uwanja wa Uhuru. 
  Siku moja baadaye, Jumapili mahasimu wao, Yanga nao wakashinda 4-0 dhidi ya wenyeji, Stand United Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  Na sasam, zote Simba na Yanga zinafungana kwa pointi 15 kila moja kileleni mwa Ligi Kuu, sawa na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA WAFURAHIA KAMBI NZURI MTONI MARINE, HOTELI YA KISASA ZAIDI ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top