• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 29, 2017

  MTIBWA SUGAR KUREJEA KILELENI LIGI KUU LEO?

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MTIBWA Sugar inaweza kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo kama itashinda dhidi ya Singida United.
  Wakata Miwa hao wa Manungu wanawakaribisha Singida waliopanda Ligi Kuu msimu huu kwenye Uwanja wa Manungu Arena, Morogoro kuanzia Saa 10:00 jioni.
  Na baada ya mahasimu wa jadi, Simba na Yanga kumalizana kwa sare ya 1-1 jana Uwanja wa Dar es Salaam na wote kufikisha pointi 18 baada ya mechi nane, wastani wa pointi mbili kwa mcheszo, Mtibwa wanahitaji kushinda kurudi juu.
  Kwa sasa, Mtibwa Sugar ya kocha Zuberi Katwila ina pointi 15, baada ya kucheza mechi saba, maana yake ikishinda leo itafikisha pointi 18.
  Mtibwa Sugar inaweza kupanda kileleni mwa Ligi Kuu leo ikishinda dhidi ya Singida United

  Lakini hilo halitarajiwi kuwa jepesi mbele ya Singida, inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm ambayo ni mshindani kweli.
  Kwa ujumla, Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea leo baada ya mechi mbili za Raundi ya nane kuchezwa juzi na jana, nyingie Azam FC wakiifunga Mbeya City 1-0 Ijumaa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Mechi nyingine za leo, Maji Maji wanaikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Lipuli FC wanaikaribisha Mbao FC Uwanja wa Samora mjini Iringa, Kagera Sugar wanaikaribish Ndanda FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Njombe Mji FC wanaikaribisha Stand United Uwanja Saba Saba, Njombe na Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine mjini Iringa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR KUREJEA KILELENI LIGI KUU LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top