• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 29, 2017

  MTIBWA YASHINDWA KUZISHUSHA SIMBA, YANGA, YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA SINGIDA UNITED MANUNGU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MTIBWA Sugar imeshindwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Singida United jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 16 sawa na Simba, Yanga na Azam FC zinazofuatana nafasi tatu za juu, zikipishana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
  Katika mchezo wa leo, Singida United walionekana kabisa kudhamiria kutopoteza mechi Manungu wakikamilisha mechi tatu za kucheza ugenini bila kupoteza hata moja.
  Hii inamaanisha Watanzania msimu huu watashuhudia msimu mzuri wa Ligi Kuu, kutokana na ushindani huu kama utaendelea.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Lipuli wameifunga 2-1 Mbao FC Uwanja wa Samora mjini Iringa, Kagera Sugar wameshinda 2-1 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Njombe Mji FC wametoa sare ya 0-0 na Stand United Uwanja wa Saba Saba na Maji Maji FC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Mwadui FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea. 
  Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Benedictor Tinocco, Rodgers Gabriel, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Dickson Daudi, Shaaban Nditi, Salum Kihimbwa, Mohammed Issa, Kelvin Sabato, Stahmili Mbonde na Ally Makarani. 
  Singida United; Peter Manyika, Michael Rusheshangonga, Shafiq Batambuze, Salum Kipaga, Juma Kennedy, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Tafadzwa Kutinyu, Nhivi Simbarashe, Danny Usengimana na Salum Chukwu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA YASHINDWA KUZISHUSHA SIMBA, YANGA, YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA SINGIDA UNITED MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top