• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 29, 2017

  WYDAD YATOA SARE NA AHLY 1-1 MISRI FAINALI YA KWANZA

  TIMU ya Wydad Casablanca jana imelazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Al Ahly katika fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, Misri.
  Wafalme hao wa mataji Morocco, walipata bao lao muhimu la ugenini kuelekea mchezo wa marudiano Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca, Misri.
  Moamen Zakaria alianza kuwafungia wenyeji Al Ahly dakika ya tatu kabla ya Wydad, mabingwa wa michuano hiyo mwaka 1992 kusawazisha dakika ya 16 kupitia kwa Achraf Bencharki.
  Mabingwa wa rekodi wa mkichuano hiyo mara nane, Ahly sasa watalazimika kwenda kushinda ugenini ili kutwaa taji la tisa Jumamosi ijayo.
  Kikosi cha Al Ahly jana kilikuwa: Ekramy; Fathy, Nagiub, Saad, Maaloul, El-Sulaya, Rabia/Hamoudi dk78, Zakaria, Abdallah, Ajayi/Soliman dk65/Moteab dk86 na Azarou.
  Wydad: Laaroubi, Rabeh, Ouattara, Noussir, Saidi, El Karti, Nakach, Gaddarine, Bencharki, Ounajem/Khadrouf dk27 na El Haddad/Doa dk83.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WYDAD YATOA SARE NA AHLY 1-1 MISRI FAINALI YA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top