• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 25, 2017

  HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOMDHIBITI AJIB MECHI YA NGAO, JUMAMOSI ITAKUWAJE?

  Beki wa Simba, Salim Mbonde akimzuia kwa mkono mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib asikamilishe mpango wake wa kumpiga chenga ya kumzunguka katika mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Ibrahim Ajib akijitahidi kujinasua kwenye mkono wa Salim Mbonde auwahi mpira katika mchezo ambao ilishinda kwa penalti baada ya sare ya 0-0
  Salim Mbonde hapa akiondosha mpira kwenye hatari dhidi ya Ibrahim Ajib. Wakati timu hizo zitamenyana tena Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Mbonde hatakuwepo kutokana na kuwa majeruhi
  Agosti 23 Ibrahim Ajib aliwekewa ulinzi mkali na wachezaji wa Simba, hapa akikwatuliwa na Muzamil Yassin
  Ibrahim Ajib hapa akiwatoka Erasto Nyoni na Haruna Niyonzima
  Ibrahim Hajib hapa amewaunga msafara Method Mwanjali na Ally Shomari
  Hapa Ibrahim yuko chini ya uangalizi wa Method Mwanjali. Jumamosi itakuwaje?
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOMDHIBITI AJIB MECHI YA NGAO, JUMAMOSI ITAKUWAJE? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top