• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 24, 2017

  RONALDO NA MESSI HADI HAWAKUPIGIANA KURA FIFA

  UPINZANI wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi umejionyesha wazi baada ya wanasoka hao kutopigiana kura katika kinyang'anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa FIFA wa Mwaka.
  Ronaldo amewashinda wote Messi na Neymar na kutwaa uanasoka bora wa dunia jana, wakati Zinedine Zidane ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Dunia mwaka 2017 katika sherehe zilizofanyika mjini London.
  Kocha na mchezaji wa Real Madrid wote waliisaidia mno timu hiyo kutwaa mataji ya La Liga na Ligi ya Mabingwa msimu uliopita. 
  Ronaldo na Messi wote walipata nafasi ya kupiga kura kuwakilisha nchi zao kuchagua wanasoka bora wa dunia, lakini wote hawajupigiana kura.
  Wakati Ronaldo alimchagua mchezaji mwenzake wa Real Madrid, beki Sergio Ramos, Messi alimchagua mchezaji mwenzake wa Barcelona, Andres Iniesta. 
  Karatasi hii inaonyesha Messi na Ronaldo hawakupigina kura PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO NA MESSI HADI HAWAKUPIGIANA KURA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top