Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
YANGA SC imeingia kambini jioni ya leo katika hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, kariakoo, Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia mwishoni mwa wiki.
Yanga SC wataikaribisha Etoile Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
Na kikosi cha Mholanzi, Hans van der Pluijm baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana mchezo wa Ligi Kuu, leo kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wa mashindano ya pili kwa ukubwa Afrika.
Yanga SC inataka kuhamishia mazoezi yake Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia kesho- ila kama itashindikana timu itaendelea kujifua Uwanja wa Karume.
Wachezaji wote wakiwemo majeruhi kama Kpah Sherman, Salum Telela na Edward Charles wameingia kambini kujiandaa na mchezo huo.
Mchezo huo utachezeshwa na marefa kutoka Msumbiji ambao ni Samuel Chirindza atakayepuliza filimbia akisaidiwa na wapeperusha vibendera, Arsenio Chadreque Marengula na Celio de Jesus Mugabe.
Yanga SC wanaanzia nyumbani kwa mara ya tatu mfululizo katika michuano hiyo, na baada ya awali kuzitoa BDF XI ya Botswana na FC Platinum ya Zimbabwe, Jumamosi watavaana na Etoile ya Tunisia.
Katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Mbeya City jana, mabao ya Yanga SC yalifungwa na Kpah Sherman, Salum Telela na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

.png)
0 comments:
Post a Comment