• HABARI MPYA

    Monday, April 13, 2015

    KAGERA SUGAR YAUA 2-0 NA SASA YAZITISHIA AMANI SIMBA, AZAM

    KAGERA Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting jioni ya leo Uwanja wa Kambarage, Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, anaripoti Phillipo Chimi kutoka Shinyanga.
    Mabao ya Kagera katika mchezo huo yamefungwa na Victor Hangaya dakika ya 45 na Atupele Green dakika ya 49.
    Kagera Sugar sasa inafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 22 na kuendelea kukamata nafasi ya nne, nyuma ya Simba SC wenye pointi 35 za mechi 21.
    Yanga SC wapo kileleni kwa pointi zao 46 za mechi 21, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 38 za mechi 21. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAUA 2-0 NA SASA YAZITISHIA AMANI SIMBA, AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top