CHELSEA imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa vijana chini ya umri wa miaka 19, baada ya kuifunga mabao 3-2 Shakhtar Donetsk nchini Uswisi.
Nahodha wa Chelsea, Izzy Brown alifunga bao la kwanza dakika ya saba kabla ya beki wake, Andreas Christensen kujifunga kuwasawazishia wapinzani dakika ya 37.
Dominic Solanke akaifungia Chelsea bao la pili dakika ya 47 kabla ya Brown kufunga la tatu dakika ya 55.
Viktor Kovalenko aliyetokea benchi, aliifungia Shakhtar bao la pili dakika ya 90 na ushei na hadi mwisho, The Blues wakabeba taji kwa ushindi wa 3-2.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Collins; Aina, Christensen, Clarke-Salter, Dasilva, Loftus-Cheek, Colkett, Brown, Musonda/Abraham dk84, Boga/Palmer dk71 na Solanke.
Shakhtar Donetsk; Kudryk, Kyryukhantsev, Sahutkin, Mayviyenko, Hladchenko, Vachiberadze, Pikhalonok, Arendaruk/Merkushov dk78, Zubkov, Shtander/Kovalenko dk71 na Boryachuk.
Wachezaji wa Chelsea U19 wakisheherekea ubingwa wa Ulaya leo baada ya kuifunga Shakhtar nchini Uswisi
Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3037207/Chelsea-U19s-3-2-Shakhtar-Donetsk-U19s-Captain-Izzy-Brown-stars-brace-Blues-claim-UEFA-Youth-League-title.html#ixzz3XDQ4ejFQ
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook


.png)
0 comments:
Post a Comment