YANGA SC wamekwenda hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika, kufuatia kuwatoa FC Platinum ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 5-2.
Yanga SC iliwastaajabisha wengi kwa ushindi wa 5-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki mbili zilizopita katika mchezo wa kwanza, kabla ya jana kufungwa 1-0 ugenini.
Na sasa, Yanga SC inasubiri mshindi wa jumla wa mchezo kati ya Etoile du Sahel ya Tunisia na Benfica ya Luanda, ili ikutane nayo katika hatua ijayo.
Etoile ilianza na ushindi mwembamba wa 1-0 nyumbani, ambao leo itapambana kuulinda mjini Luanda ili kusonga mbele. Yanga inaweza kukutana na timu yoyote kati ya hizo.
Kwa dhati kabisa, tena bila woga nichukue fursa hii kuwapongeza Yanga SC kwa matokeo haya.
Tumezoea, Yanga SC inapotoka kufungwa na Simba SC, basi kinachofuata ni vurugu tupu, ambazo mwisho wa siku zinaathiri hadi matokeo ya uwanjani katika mechi nyingine.
Yanga SC iliingia kucheza na Platinum mchezo wa kwanza, ikitoka kufungwa 1-0 na mahasimu wao wa jadi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Maneno maneno yalikwishaanza, na baadhi ya wachezaji walisumbuliwa na wanachama ambao bado wana fikra mgando.
Watu walimvamia winga Simon Msuva wanataka kumpiga eti amecheza kinazi- kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ naye alikuwa katika wakati mgumu kwa kufungwa bao lililoonekana rahisi na Emmanuel Okwi.
Haruna Niyonzima, Danny Mrwanda, Kevin Yondan na Msuva wote walikuwa katika wakati mgumu baada ya matokeo hayo.
Ilikuwa vurugu tupu na binafsi nilianza kupata wasiwasi, kama hali hiyo itaendelea na Yanga SC ina mechi ya Kombe la Shirikisho wiki inayofuata, itakuwaje?
Lakini siku ya kwanza ya wiki kuelekea mwishoni mwa wiki ya mchezo wao na Platinum, nilikwenda kwenye mazoezi ya Yanga SC Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na nilichokikuta kilinifurahisha sana.
Makocha Mholanzi, Hans van der Pluijm na Msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa waliweza kuwaunganisha wachezaji mara moja na kuwasahaulisha yaliyopita.
Yanga SC walikuwa wanaendelea na mazoezi yao kwa furaha kabisa kana kwamba hakuna kilichotokea, zaidi wakiifikiria mechi iliyo mbele yao.
Hata maisha ya kambini kwa wachezaji yalikuwa salama kabisa- ni makocha na wachezaji wao tu wakijiandaa kwa mechi.
Haikuwa ajabu kwa hali kama hiyo, Yanga SC wakaipiga 5-1 Platinum na tangu hapo hawajafungwa tena mechi hata kwenye Ligi Kuu.
Yanga SC iliifunga 2-1 Kagera Sugar, 2-0 Mgambo JKT na 3-1 JKT Ruvu baada ya kuilaza 5-1 Platinum na sasa inaongoza Ligi Kuu.
Na baada ya jana kuitoa Platinum, Yanga SC wanafikiria mambo mawili tu sasa, ubingwa- na namna ya kusonga mbele zaidi Kombe la Shirikisho.
Yanga SC ni klabu ambayo ipo tangu enzi za ukoloni na itaendelea kuwapo, ikipitia matokeo yote, kushinda na kushindwa.
Na kuna kipindi itapitia katika wakati mgumu wa ukame wa mataji, kisha itasimama imara tena, hivyo ndivyo soka ilivyo. Hata Man United baada ya kutamba sana England na Ulaya enzi za Sir Akex Ferguson, sasa hivi wanajitutumua.
Huwezi kuwa mfalme milele, aliwahi kusema bingwa wa zamani wa ndondi za uzito wa juu duniani, Mike Tyson na katika soka timu haiwezi kushinda kila siku.
Barcelona kila siku ni bora, lakini haishindi kila mechi na haichukui mataji kila msimu.
Niseme wazi, safari hii Yanga SC wamenifurahisha kwa kuonyesha ukomavu wa hali ya juu- baada ya kufungwa na mahasimu, walitulia bila kuvurugana na kupeleka nguvu zao kwenye michuano ya Afrika, sasa wanafurahia matokeo mazuri katika mashindano makubwa. Nani anaifikiria Simba SC kwa sasa? Yanga wanawaza ubingwa na jinsi gani watawatoa Etoile, au Benfica. Hongera zenu wana Jangwani.

.png)
0 comments:
Post a Comment