MBABE mpya wa ndondi za uzito wa juu, Anthony Joshua amemsimamisha mpinzani wake, mzoefu Jason Gavern wa Marekani kwa Knockout (KO) raundi ya tatu katika pambano lisilo la ubingwa mjini Newcastle.
Hata hivyo, bondia huyo wa Uingereza anayeitwa 'Lennox Lewis mpya' pamoja na kushinda pambano la 11 mfululizo tangu aanze ndondi za kupigana kifua wazi, hakufurahishwa na kiwango chake akisema hakuwa katika ubora wake jana.
Gavern, akipigana pambano lake la 50, aliangushwa mara mbili katika raundi ya pili na akaangushwa tena katika raundi ya tatu pambano hilo likiishia hapo.
Sasa, Joshua, ambaye alirejea ulingoni baada ya kukosekana kwa miezi mitano kutokana na majeruhi ya mgongo, atapambana na Kevin Johnson ukumbi wa O2, London Mei 30.
Anthony Joshua akimchapa konde mpinzani wake, Jason Gavern
Joshua akimuadhibu mpinzani wake mjini Newcastle jana
Joshua akiwa amesimama mbele ya Gavern aliyeanguka chini
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-3025978/Anthony-Joshua-stops-Jason-Gavern-warm-Kevin-Johnson-test.html#ixzz3WPElKVek


.png)
0 comments:
Post a Comment