TIMU ya Maveterani wa Simba SC, jana imewafunga maveterani wa Azam FC bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Bao pekee la maveterani wa Simba SC limefungwa na mshambuliaji Bita John Musiba katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua kuazimisha sherehe za Pasaka.
Kabla ya kuanza kwa mchezo huo, vikosi vya timu zote mbili vilisimama kwa dakika moja kuomboleza msiba wa wanachama sita wa Simba SC waliofariki ajalini Morogoro juzi wakiwa njiani kuelekea Shinyanga kuishangilia timu yao katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Issa Manofu, Barnabas Sekelo/Idd Suleiman ‘Meya’, Twaha Hamidu ‘Noriega’, Said Kokoo, George Masatu, Khalid Abeid, Shauri Idd/Robert Damian, Yusuph Macho, Bitta John, Dua Said na Itutu Kigi ‘Road Master’/Thomas Kipese ‘Uncle Thom’.
Azam FC; Iddi Ramadhan, Mussa Lumbi, Omar Cantona, Ramadhan Juma, Abdallah Kassim, Habib Kondo, Hussein Bado, Jemedari Said, Nassor Idrisa ‘Father’, Abdulkarim Amin na Dahoma Uki.

![]() |
| Wachezaji wa SImba na Azam wakisalimiana kabla ya mechi |
![]() |
| Wachezaji wa timu zote mbili walisimama kwa dakika moja kuomboleza vifo vya wanachama wa Simba |

.png)
0 comments:
Post a Comment