• HABARI MPYA

    Thursday, April 02, 2015

    TIMU YA TAIFA NDONDI YATAJWA, ITASHIRIKI MICHUANO KIBAO YA KIMATAIFA

    HATIMAYE baada ya mchakato wa muda mrefu, uliofanyika kwa umakini kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa hatimaye Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) limepata wachezaji wa timu ya Taifa ya Ngumi 2015. 
    Katibu wa BFT, Makore Mashaga amesema timu hiyo imepatikana baada ya mashindano ya kimataifa yaliyoshirikisha timu za taifa kutoka Uganda na Kenya, yaliyomalizika kwa mafanikio Machi 28, mwaka 2015.
    Amesema mabondia waliochaguliwa kwa sasa taratibu za kuombewa ruhusa katika timu zao zinafanyika na taratibu hizo zitakapo kamilika watatakiwa kuanza mazoezi kabla ya Aprili 15, 2015, kwa ajili ya kushiliki mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa hasa mashindano ya Michezo ya Afrika kati ya Septemba 4 na 19 mjini Brazzaville, Kongo na mashindano ya Ubingwa wa Dunia kuanzia Oktoba 5 hadi 18 mjini Doha, Qatar.

    Mabondia waliochaguliwa na uzito wao ni kama ifuatavyo:-
    Light Flya; Mohamed Mzeru (JKT), Maulid Athumani, Ibrahim Abdalah (Magereza), Fly; Juma Ramadhani (Temeke), Said Hofu (JKT), Bantam; Ahamad Furahisha (JKT), Bon Mlingwa (JKT).
    Light; Elias Mkomwa (JKT), Bosco Bakari (JKT), Fabian Gaudence (NGOME), Light; Kassim Mbwitike (JKT), Welter Weight, Said Gulushad (JKT), Seleman Bamtulah (JKT), Middle, Ivan Mussa (Kagera) Light Heavy; Hamidu Halfan (JKT), Heavy, Alex Sitta (JKT) na Nuru Ibrahim (Magereza).
    Aidha BFT, inawapongeza mabondia wote kwa jitihada kubwa walizofanya na hatimaye kuchaguliwa kuwa mabondia wa timu ya taifa ya ngumi 2015.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU YA TAIFA NDONDI YATAJWA, ITASHIRIKI MICHUANO KIBAO YA KIMATAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top