• HABARI MPYA

    Sunday, June 14, 2026

    SCOTLAND YAILAZA HAITI 1-0 KOMBE LA DUNIA

    TIMU ya Scotland imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Haiti katika mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Dunia Alfajiri ya leo Uwanja wa Gillette mjini Foxborough, Norfolk County, Massachusetts, Marekani. 
    Hongera zake mfungaji wa bao hilo pekee, Nahodha na kiungo wa Aston Villa ya England, John McGinn dakika ya 28 hilo likiwa bao lake la 21 timu ya taifa katika mechi ya 87.
    Mechi nyingine ya kwanza ya Kundi C jana Brazil ilitoa sare ya kufungana bao 1-1 na Morocco Uwanja wa MetLife mjini East Rutherford, New Jersey Jijini New York, Marekani. 
    Kiungo wa PSV Eindhoven ya Uholanzi, Ismael Saibari mzaliwa wa Hispania alianza kuwafungia ‘mabingw awa mezani’ wa Afrika, Morocco dakika ya 21, kabla ya mshambuliaji wa Real Madrid, Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior kuisawazishia Brazil dakika ya 32.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SCOTLAND YAILAZA HAITI 1-0 KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top