Na Mahmoud Zubeiry, DARA ES SALAAM
KIUNGO tegemeo wa Yanga SC, Salum ‘Master’ Telela anapambana na maumivu ya kifundo cha mguu ili kupona na kuuwahi mchezo dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia mwishoni mwa wiki.
Yanga SC watakuwa wenyeji wa Etoile Aprili 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
Na Telela aliumia kifundo cha mguu jana baada ya kuchezewa rafu na mshambuliaji wa Mbeya City, Thelix- ambaye alitolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.
Telela anayeinogesha safu ya kiungo ya Yanga SC kwa sasa, alishindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake ikachukuliwa na Hassan Dilunga.
Baada ya mchezo huo, Telela aliimbia BIN ZUBEIRY kwamba amepata maumivu ya kifundo cha mguu ambayo anahisi ni makali.
“Si maumivu madogo, ila sijui hali itaendeleaje, ngoja nisikilize siku mbili hizi, ila kwa sasa hali si nzuri,”alisema.
Telela aliumia na kutoka nje akiwa tayari amefunga bao moja katika ushindi wa 3-1 jana, mabao mengine ya Yanga SC yakifungwa na Kpah Sherman na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati la City lilifungwa Themi Felix.

![]() |
| Salum Telela ameumia enka ya mguu wa kushoto |
Baada ya mchezo huo, Telela aliimbia BIN ZUBEIRY kwamba amepata maumivu ya kifundo cha mguu ambayo anahisi ni makali.
“Si maumivu madogo, ila sijui hali itaendeleaje, ngoja nisikilize siku mbili hizi, ila kwa sasa hali si nzuri,”alisema.
Telela aliumia na kutoka nje akiwa tayari amefunga bao moja katika ushindi wa 3-1 jana, mabao mengine ya Yanga SC yakifungwa na Kpah Sherman na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati la City lilifungwa Themi Felix.

.png)
0 comments:
Post a Comment