Na Vincent Malouda, NAIROBI
TIMU ya KCB anapochezea japo kwa mkopo straika la Simba SC Raphael Paul Mungai Kiongera ililazwa magoli 3-1 na bingwa mtetezi ligi kuu Kenya, Gor Mahia katika mechi ya ligi usiku wa Jumatano katika uwanja wa taifa wa Nyayo.
Mzawa wa Uganda mwenye uraia wa Rwanda Meddie Kagere alicheka na nyavu mara mbili huku mzawa mwingine wa Uganda na raia wa Kenya Innocent Wafula akimalizia magoli ya Gor Mahia dakika ya 55 baada ya Victor Majid kuipa KCB bao lao la pekee dakika ya 52.
Kagere alifungua nyavu za wapinzani dakika moja baada ya mwamuzi Amos Ichingwa kupuliza kipienga akimalizia pasi ya Ali Abondo. Beki wa KCB Kelvin Omondi alikuwa amezubaa kuondoa uchafu langoni na kumruhusu Abondo kumpokonya mpira.
Wanabenki hawakuonyesha ari yoyote ya kuzawazisha pale Kagere aliumiza nyoyo zao na bao la pili dakika ya 40 akipokea krosi ya Michael Olunga kutoka pembeni na kuwekeza ngoma kwenye mlango wa kipa Zachary Onyango.
Kipindi cha pili, vijana wake Rishadi Shedu walianza vyema wakibisha langoni mwa K'Ogalo lakini mlindamlango Boniface Oluoch alifanya kilichomleta Gor kutoka Tusker. Hata hivyo, Oluoch alishindwa kuzuia shuti la Majid dakika ya 52 kutoka katikati mwa uwanja kwenye hikabu iliyosababishwa na Ronald Otieno kumchezea mazihara Benjamin Chaka. Dakika tatu baadaye,Wafula aliwapa halaiki ya mashabiki wa Gor wanachopenda kwa kufunga bao la tatu na lake la kwanza tangu kujiunga nao mwanzoni mwa msimu kutoka Chemelil Sugar.
Kwa ushindi huo, vijana wa Msikochi Frank Nuttal wanapaa kileleni mwa jedwali kwa alama 12 baada ya mechi nne huku KCB ambao bado wanazikosa huduma za Kiongera aliyeanza mazoezi ya uwanja nao wakisalia nafasi ya 14 kwa pointi tatu tu wakiwa wamewajibikia ngarambe tano.
Awali, Sofapaka ilikamatwa 1-1 na Muhoroni Youth uwanjani Muhoroni. Beki Collins Shivachi akizawazisha bao la Muhoroni lilofungwa na raia wa Nigeria Abbas Akinyemi dakika ya 11.

![]() |
| Paul Kiongera yupo kwa mkopo KCB kutoka Simba SC |

.png)
0 comments:
Post a Comment