• HABARI MPYA

    Monday, April 13, 2015

    ALLIANCE FC YAJIANDAA NA LIGI YA KANDA

    Na Alex Sanga, MWANZA
    Kocha wa Msaidizi wa Timu ya Alliance Fc ya mkoani hapa kessy Mziray amesema kuwa timu yake kwa sasa inajiandaa na Maandalizi makubwa na Ligi ya Kanda ya Ziwa inayoanza mei mwaka huu.
    Kessy alisema kwa sasa wanafanya mazoezi ya ufukweni na gym ila wiki ijayo wataanza mazoezi ya uwanjani.
    Mabingwa hao wa mkoa msimu huu wa 2014-2015 wapo pia katika Maandalizi ya kwenda nchini kenya kucheza na vigogo wa huko, Sofapaka B na Gor Mahia.


    Mkurugenzi wa Alliance Football Club, James Bwire amemchagua kocha wa zamani wa timu ya Hekima,Mkolani na Nange Fc Mathias Wandiba awe kocha Mkuu wa timu ya Under 17 ya Alliance.
    Alliance FC ndio Mabingwa wa Mkoa wa Mwanza na timu yao imefuzu katika kucheza Ligi ya Kanda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALLIANCE FC YAJIANDAA NA LIGI YA KANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top