• HABARI MPYA

    Thursday, April 16, 2015

    HAZARD, HARRY KANE WAWAFUNGA TELA DIEGO COSTA, DE GEA NA SANCHEZ TUZO ZA PFA 2015

    NYOTA wa Chelsea, Eden Hazard na Harry Kane wa Tottenham Hotspur wanaongoza mbio za tuzo za Mwanasoka Bora wa Mwaka wa PFA msimu wa 2014-15. Washambuliaji wa Chelsea, Diego Costa, Alexis Sanchez wa Arsenal, David de Gea wa Manchester United na Philippe Coutinho wa Liverpoool nao pia wamo kwenye orodha ya mwisho ya wachezaji sita wanaowania tuzo hiyo.
    Hazard amekuwa katika kiwango kizuri msimu wote Stamford Bridge, akiiongoza Chelsea kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mabao yake 12 na pasi tisa za mabao.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, mwaka jana alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora Chipukizi wa PFA, akiiwezesha Chelsea kutwaa taji la Capital One pamoja na mshambuliaji Costa, ambaye alifunga mabao 20 katika msimu wake wa kwanza England.
    Harry Kane's prolific form for Tottenham has seen him nominated for PFA Player of the Year
    Harry Kane anaongoza katika mbio za tuzo za PFA
    Diego Costa (right) scores for Chelsea in the Capital One Cup final victory over Tottenham at Wembley
    Diego Costa (kulia) aliifungia Chelsea katika fainali ya Capital One dhidi ya Tottenham Uwanja wa Wembley
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAZARD, HARRY KANE WAWAFUNGA TELA DIEGO COSTA, DE GEA NA SANCHEZ TUZO ZA PFA 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top