• HABARI MPYA

    Monday, July 06, 2026

    BELLINGHAM APIGA MBILI ENGLAND YAICHAPA MEXICO 3-2


    TIMU ya England imefanikiwa kutinga Hatua ya Robo Fainali Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji wenza, Mexico Asubuhi ya leo Uwanja wa Azteca Jijini Mexico City nchini Mexico.
    Kiungo wa Real Madrid ya Hispania, Jude Victor William Bellingham mwenye asili ya Ireland kupitia kwa baba yake na Kenya kupita kwa mama yake aliifungia Three Lions mabao mawili dakika ya 36 na 38, kabla ya Nahodha Harry Edward Kane kufunga la tatu kwa penalti dakika ya 60.
    Mabao ya Mexico ambao wanakuwa wenyeji wa pili kutolewa baada ya Canada waliochapwa 3-0 na Morocco juzi – yamefungwa na washambuliaji, Julián Andrés Quiñones Quiñones wa Al-Qadsiah ya Saudi Arabia mzaliwa wa Colombia dakika ya 42 na Raúl Alonso Jiménez Rodríguez wa Wolverhampton Wanderers ya England dakika ya 69 kwa penalti.
    England sasa watamenyana na Norway ambayo usiku wa jana nayo ilitinga Robo Fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brazi usiku wa kuamkia leo Uwanja wa MetLife Jijini East Rutherford, New Jersey, New York, Marekani.

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BELLINGHAM APIGA MBILI ENGLAND YAICHAPA MEXICO 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top