TIMU ya Colombia imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Ghana Asubuhi ya leo Uwanja wa Arrowhead Jijini Kansas City, Missouri, Marekani.
Bao pekee lilliloipa ushindi Colombia limefungwa na kiungo mshambuliaji wa Palmeiras ya Brazil, Jhon Adolfo Arias Andrade aliyefundishwa soka katika akademi za Dorados na Tijuana nchini Mexicio – ambaye alifunga dakika ya 14.
Colombia inakamilisha idadi ya timu 16 za hatua inayofuata ya Fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu zinazoandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Canada, Marekani na Mexico.
Nyingine ni Argentina, Canada, Morocco, Paraguay, Ufaransa, Brazil, Norway, Mexico, England, Ureno, Hispania, Marekani, Ubelgiji, Misri na Uswisi.



.png)
0 comments:
Post a Comment