• HABARI MPYA

    Friday, April 17, 2015

    NAPOLI YAIKUNG’UTA 4-1 WOLFSBURG KWAO UJERUMANI ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE

    TIMU ya Napoli ya Italia, imeifumua Wolfsburg mabao 4-1 Uwanja wa Volkswagen usiku wa kuamkia leo katika Robo Fainali ya kwanza ya Europa League.
    Gonzalo Higuain aliwafungia wageni bao la kwanza dakika ya 15, kabla ya Marek Hamsik kufunga la pili dakika ya 23.
    Higuain akamsetia Hemsik kufunga bao la tatu dakika ya 64 na Manolo Gabbiadini akafunga la nne dakika ya 77, kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Nicklas Bendtner kuwafungia wenyeji bao la kufutia machozi dakika ya 80.
    Kikosi cha Wolfsburg kilikuwa; Benaglio, Vieirinha, Naldo, Knoche, Rodriguez; Guilavogui/Arnold dk70, Luiz Gustavo, Caligiuri, De Bruyne, Schurrle/Perisic dk64 na Dost/Bendtner dk57.
    Napoli; Andujar, Maggio, Albiol, Britos, Ghoulam; David Lopez, Inler, Callejon, Hamsik/Gabbiadini dk75, Mertens/Insigne dk60, Higuain/Henrique dk86.
    Katika mechi nyingine za Dynamo Kyiv imetoka sare ya 1 – 1 na Fiorentina Uwanja wa Olimpiki,  bao lake likifungwa na Jeremain Lens dakika ya 36 na Khouma Babacar akiwafungia wapinzani dakika ya 92.
    Club Brugge imetoka sare ya  0 – 0 na Dnipro Dnipropetrovsk Uwanja wa Jan Breydel, Sevilla imeifunga 2-1 Zenit St Petersburg mabao yake yakifungwa na Carlos Bacca dakika ya 73 na Denis Suarez dakika ya 87, huku la wapinzani wao likifungwa na  Aleksandr Ryazantsev dakika ya 29 Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan.
    Marek Hamsik celebrates with team-mates after making it 3-0 to Napoli in the first leg of the quarter-final
    Marek Hamsik akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la tatu katika ushindi wa 4-1 wa Napoli 

    PICHA ZAIDI NENDA: 

    http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3042621/Wolfsburg-1-4-Napoli-Marek-Hamsik-nets-brace-Rafa-Benitez-s-run-riot-Europa-League-quarter-final-leg.html#ixzz3XWNTqfR7 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAPOLI YAIKUNG’UTA 4-1 WOLFSBURG KWAO UJERUMANI ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top