RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo amemtembelea na kumpa pole kiungo Muivory Coast wa Yanga SC, Peodoh Pacome Zouzoua, ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.
Pacome aliumia katika mchezo wa kufungia msimu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Juni 30, Yanga ikishinda 3-0 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam na kutwaa ubingwa kwa mara ya tano mfululizo.


.png)
0 comments:
Post a Comment