KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal jana amesherehekea ushindi wake wa 4-2 dhidi ya mahasimu, Manchester City kwa staili ya aina yake baada ya kupigwa picha akiwa na wachezaji wa timu ya wanawake ya Manchester City, Toni Duggan na Isobel Christiansen katika mgahawa.
Duggan ameposti picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa na Christiansen na Michelle Hinnigan wa Eveton katika mgahawa wa kichina wa Wing, kufuatia ushindi wa United wa 4-2 dhidi ya wapinzani wao wakubwa, City, na kuandika: "Heyyy Louis van G!!!! Nzuri kushea na wewe...... [sic].". Duggan baadaye akafuta posti hiyo.
Wing ni sehemu ambayo wanasoka wanapenda kwenda mjini Manchester, miongoni mwao akiwa ni Nahodha wa England na United, Wayne Rooney, lakini wachezaji pekee wa City walionaswa nu Duggan na Christiansen.
Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amepigwa picha akiwa na wachezaji wa timu ya wanawake ya Manchester City, Toni Duggan (kushoto) na Isobel Christiansen (kulia kabisa) na Michelle Hinnigan wa Everton katika mgahawa wa Wing kusherehekea ushindi wa 4-2 jana dhidi ya mahasimu wake hao katika Ligi Kuu ya England.
Louis van Gaal akiondoka katika mgahawa wa Wing's baada ya kula bata na rafiki zake hao
Van Gaal alikuwa katika mgahawa huo kufurahi pamoja na mkewe, Truss na rafiki zake
PICHA ZAIDI NENDA:
http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3036546/Louis-van-Gaal-celebrates-Manchester-derby-win-restaurant-snapped-CITY-women-s-players-Juan-Mata-Daley-Blind-Ander-Herrera-hit-town-too.html#ixzz3XCcMVPDH


.png)
0 comments:
Post a Comment