WINGA Ashley Young yuko radhi kupunguziwa mshahara, lakini aendelee kuichezea Manchester United.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 amefufua makali yake siku za karibuni chini ya kocha Louis van Gaal na kufanikiwa kurejesha nafasi yake katika wingi ya kushoto.
Ashley Young alifunga Jumapili katika ushindi wa 4-2 dhidi ya mahasimu Manchester City
Young amekuwa chachu ya matokeo mazuri ya United katika mechi sita zilizopita na sasa anatazamiwa kurejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England.
United iliipiku Liverpool katika kuwania saini ya Young akiwa Aston Villa kwa dau la Pauni Milioni 17 mwaka 2011 na ikampa Mkataba wa miaka mitano kwa mshahara wa Pauni 120,000 kwa wiki.
Anatarajia kuongezewa Mkataba wa miaka mitatu na yuko tayari kupunguziwa mshahara, huku wawakilishi wake wakijipanga kwa mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward wiki zijazo.


.png)
0 comments:
Post a Comment