// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); COASTAL UNION WAIANDALIA SHUGHULI PEVU JKT RUVU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE COASTAL UNION WAIANDALIA SHUGHULI PEVU JKT RUVU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, January 01, 2015

    COASTAL UNION WAIANDALIA SHUGHULI PEVU JKT RUVU

    Na Oscar Assenga, TANGA
    TIMU ya Coastal Union imeanza maandalizi kabambe ya kuhakikisha inajipanga vema ili kuhakikisha timu hiyo inapata pointi tatu muhimu
    kwenye mechi yake ya Ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kutokana na umahiri wa kikosi cha timu hiyo.
    Akizungumza  leo mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly, Ofisa
    Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prison tayari Kocha wao mkuu Mkenya  James Nandwa alikwisha kuyafanyia kazi na sasa kikosi kipo kamili kuwavaa maafande hao.

    Amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni mzuri kwa sababu tayari,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Mkenya James Nandwa alikwisha fanyia kazi kubwa ya kukiandaa timu hiyo na ataingia kwenye mechi hiyo akiwa na lengo moja la kuhakikisha ushindi unapatikana ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara.
    Hata hivyo amesema hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi na kuwataka wapenzi na mashabiki kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION WAIANDALIA SHUGHULI PEVU JKT RUVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top